Ni agizo lake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kawe katika maadhimisho ya siku ya lishe yaliyofanyika katika viwanja ya Tanganyika Pakers leo.
Amesema jamii ndio msingi imara wa maendeleo hivyo nguvu nyingi ielekezwe kwao kwa kutoa elimu rahisi ya lishe itakayowapelekea kuwa na uelewa wa pamoja kuhusiana na umuhimu wa mlo kamili na lishe kwa afya zao.
"Wataalam tafuteni lugha rahisi ya kutoa elimu kwa watu wetu kuhusiana na lishe, hii ni muhimu sana, kwani itawasaidia kuhakikisha wanapata mlo kamili kwenye vyakula vyao, ikiwezekana tumieni majina ya rangi kwani ndio mazingira wanayoishi kwenye jamii". Amesema Mhe. Gondwe.
Aidha amesisitiza pia umuhimu wa lishe kwa wanawake wajawazito ndani ya siku mia moja tangu kupata ujauzito na siku 1,000 baada ya kujifungua, ikiwemo chanjo muhimu na kuwataka waalimu kuwasisitiza wazazi kuwa na mpango mkakati wa lishe kwa watoto wao hali itakayowaondolea udumavu uliosababishwa na kukosa mlo kamili au mlo ulio bora.
Naye Mkuu wa Idara ya Mifugo Bi. Betila Lyimo, alipotakiwa kuzungumza amesema lishe inayotokana na mifugo ni lishe imara iliyo na virutubisho muhimu mwilini inayompasa mwanadamu yeyote kutumia na kuahidi kufanyika kazi maelekezo yote hususan utoaji wa elimu ya lishe kwa jamii kwa kutumia njia iliyo rahisi ili wote kwa pamoja tuweze kuwa na afya bora ili tusukume gurudumu la maendeleo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wajasiriamali kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kuzitangaza bidhaa zao kwa kuzipa majina, rangi na nembo itakayotoa utambulisho.
Maadhimisho hayo ya lishe pia yamehudhuriwa na wadau wa lishe, viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali, Watendaji wa Kata na Mitaa, wananchi, Idara ya mifugo, wajasiriamali pamoja na wanafunzi kutoka shule ya Msingi Tumaini.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.