Walengwa na wanufaika wa TASAF wamehimizwa kurekebisha taarifa zao kila kunapotokea mabadiliko katika Kaya zao.
Hayo yalielezwa Machi 26, 2024 katika kikao cha ufatiliaji wa taarifa na upokeaji wa fedha kwa Kaya maskini katika Mitaa ya Wazo na Mivumoni, Kata Wazo.
Akizungumza na wanafaika wa mfuko huo, Bi. Teddy Kyara, aliwaomba wanufaika kuwa na tabia ya kufanya marekebisho katika taarifa zao pale kunapotokea mabadiliko kama vifo au watoto wanapopanda daraja katika ngazi ya elimu.
"Rekebisheni taarifa za watoto wetu ili wanapofika ngazi ya Chuo Kikuu wanapewa kipaumbele cha mikopo kwa asilimia mia, alisema Bi. Kyara.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.