Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amewataka wachimbaji wa mchanga katika bonde la mto Mpiji kufuata Kanuni na Sheria za uhifadhi wa Mito zilizowekwa.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo Oktoba 2, 2023, katika ziara aliyoifanya katika bonde la mto Mpiji ili kujionea shughuli zinazofanyika kama zinakidhi miongozo ya uhifadhi wa bonde iliyopo kikanuni na kisheria.
"Niwaombe watu wote wanaofanya shughuli za uchimbaji wa mchanga kwakutumia machepe na Wakandarasi katika bonde hilo na mengine pasipo kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa, kuwa watakumbana na mkono wa Sheria endapo wataendelea kufanya kazi bila utaratibu uliopo", amesema Mhe. Chalamila.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amekipongeza kikundi cha mshikamano kuwa mfano wa kuigwa, kwa kuwa kinafanya shughuli zake kihalali, kinafuata miongozo na kuchangia pato la nchi na ajira pia.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.