Kufuatia mfululizo wa mvua zinazoendelea kunyesha sehemu mbalimbali, Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Kinondoni imefanya ziara Novemba 20, 2023 Kata za Bunju na Wazo huku ikiwatahadharisha wananchi kuhama maeneo hatarishi.
Akiongea na Watendaji wa Kata hizo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Bi. Stella Msofe, amewatahadharisha Watendaji hao kuwa mvua bado zipo hivyo wazidi kuwaelemisha wananchi wanaokaa maeneo ya bondeni na pembezoni mwa mito.
"Kuna watu wengi wanaokaa kwenye maeneo ambayo siyo salama kabisa kwa kipindi hiki, tunawasihi Watendaji wa Kata waendelee kutoa elimu na tahadhari juu yao ili wahame mara moja badala ya kusubiri msaada kutoka serikalini," amesema Bi. Stella.
Kadhalika, Katibu Tawala amehimiza usafi upewe kipaumbele katika kipindi hiki cha mvua ili kuzuia mlipuko wa magonjwa unaoweza kusababishwa endapo maeneo hayatasafishwa ipasavyo na kwa muda muafaka.
"Sote kwa pamoja tushirikiane kufanya usafi kwenye maeneo yetu hasa kwenye mifereji ili turuhusu maji yapite kwa urahisi na kufanya hivyo itatusaidia sana kuondokana na changamoto hii ya kujaa kwa maji kwenye makazi yetu," amesema Bi. Stella.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.