Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amewasihi Wananchi kuendelea kuchukua tahadhali ili kuepukana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua zinaendelea kunyesha wakati huu.
Mhe. Saad ameyasema hayo leo Novemba 2, 2023 alipofanya ziara katika Kata ya Mbezi-Juu kuangalia miundombinu ya barabara na madaraja ambayo yako hatarini kuharibika ikiwa mvua zitaendelea kunyesha na kutoboreshwa.
"Taarifa za uwepo wa mvua hizi za mfululizo tulipewa mda mrefu sana na sasa zimeanza rasmi, ni wakati wa kuchukua tahadhali zote zinazotakiwa ili tusiathirike" ameongeza Mhe. Saad.
Aidha, Mhe. Saad amewaomba Wazazi na Walezi kufuatilia kwa umakini mienendo ya watoto wao maana ndio wahanga wakubwa wa athari zitokanazo na mvua ikiwepo kutowaruhusu watoto kucheza katika maeneo hatari ikiwepo maeneo ya mifereji au mito hasa kipindi hiki cha mvua.
Katika kuhakikisha Wananchi wanakuwa salama kipindi hiki cha mvua, Mhe. Saad amewasisitiza Wananchi kufanya usafi wa mitaro ili kuruhusu maji kupita na pia taarifa za uharibifu wa miundombinu zitolewe kwa uharaka na ziweze kushughulikiwa na mamlaka husika.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.