NI KUPITIA TAASISI YA ROCHAS FOUNDATION YA NCHINI NIGERIA NA TULIA TRUST YA NCHINI TANZANIA ZILIZOJIKITA KUTOA ELIMU KWA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU.
Taasisi ya Rochas Foundation nchini Nigeria, kwa kushirikiana na Tulia Trust Nchini Tanzania yaahidi kusomesha watoto yatima,na wale waishio kwenye Mazingira magumu watano kutoka shule ya Msingi makumbusho.
Akitoa ufafanuzi wa ufadhili huo Gavana wa Imo state nchini Nigeria Ndg. Rochas Owele Okorocha kwa kushirikiana na Tulia Trust amesema taasisi yake inayojishughulisha na maswala ya elimu imelenga kufadhili watoto hao, kuanzia kidato cha kwanza hadi chuo kikuu,na kwamba azma yake ni kuchukua watoto watano kila mwaka.
Naye Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Tulia Akson amesema hii ni fursa pekee kwa watoto hawa kupata elimu ambayo ndiyo msingi wa Maisha ya sasa na badae.
Alipokuwa akitoa taarifa ya changamoto zinazoikabili shule hiyo,kwa mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu Ndugu Odas Bambaza amesema shule yake inaidadi ya watoto yatima na wale waishio mazingira magumu 88, hali inayochangia utoro na kuwarudisha nyuma kitaaluma, inao pia upungufu wa vyoo, kutokuwepo na uzio wa shule, pamoja na uchakavu wa vyumba vya madarasa.
Naye Bi Dominik Chitegese kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ameishukuru Rochas foundation na Tulia trust kwa ufadhili huo wa watoto yatima na waishio kwenye Mazingira magumu, kwani kwa kufanya hivyo ni kuwajengea uwezo na kuwarudishia matumaini ya maisha hasa ikizingatiwa elimu ndio ufunguo wa maisha.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.