Wanafunzi wameaswa kutumia fursa za kujiunga kwenye klabu mbalimbali ambazo zipo shuleni zitakazowasaidia katika kukabiliana na changamoto za maisha baada ya kuhitimu masomo yao . Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Kituo cha utangazaji cha ITV Bi. Joyce Mhavile Mei, 30 2024 wakati wa utoaji wa tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kuibuka kuwa vinara katika uhamasishaji na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari Kawe Ukwamani iliyoandaliwa na Taasisi ya Wanawake Wasanifu Majenzi (TAWAH) kwa kushirikina na Kituo cha ITV, maji ya kunywa ya Kilimanjaro pamoja na Legal Aid.
"Msiache kujiunga kwenye klabu hizi kila utakachokipata chukua kimbia nacho kwani maisha ya sasa hivi sio yakutegemea ajira hivyo tumieni hizo klabu kwani zinageuka kuwa fursa."
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Kituo cha ITV ametoa tuzo kwa Wanafunzi wanne (4) walioibuka vinara katika programu ya utunzaji wa mazingira katika klabu ya WASH iliyopo katika Shule hiyo. Kwa upande wake Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwl. Amina Athumani amewapongeza Wanafunzi hao walioibuka vinara kwa kupata tuzo kwani moja ya mafanikio katika mpango wa Serikali katika Mradi wa Shule salama wenye lengo la kuhusisha na kuimarisha stadi za maisha.
"Kupitia klabu hizi za Mashuleni tunaona mafanikio kwani kupitia mradi huu wa Shule salama utawasaidia Wanafunzi katika kukabiliana na changamoto za kimaisha pindi watakapohitimu masomo yao." Mwl. Amina alisema.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.