Wanafunzi waliopo katika programu maalumu ya SEQUIP Manispaa ya Kinondoni, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwapa nafasi ya kuendelea na masomo.
Hayo yamebainika Machi 19 2024 katika mkutano na Waadishi wa habari juu ya tathmini ya miaka 3 ya uongozi wa Mhe.Samia katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 19, 2024, Afisa Elimu ya Watu Wazima Sekondari na Elimu ya Mfumo Rasmi (SEQUIP), Bi. Explancer Violet Siame, alisema,"Mimi kama Mzazi, Mwalimu na Mlezi tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwapa nafasi ya kujiendeleza tena kwani mabinti wengi wanafika mbali sasa"
Aidha, Bi. Siame alisema kuwa mwitikio wa wanafunzi hao mkubwa na wamekuwa na juhudi katika kusoma.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.