NI KUFUATIA KAMPENI YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE NCHINI TANZANIA INAYOENDESHWA NA WIZARA YA AFYA.
Hayo yamebainishwa leo na Kaimu mganga mkuu wa Manispaa hiyo Dr. Neema Mlole, alipokuwa akiendesha mafunzo ya siku moja yaliyohusisha watendaji wa Kata, waratibu wa Elimu kata, pamoja na Maafisa Afya wa Manispaa hiyo, kuhusiana na kampeni ya utoaji dawa kwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele.
Amesema, kampeni ya utoaji dawa kwa magonjwa haya, imelenga watoto wenye umri kuanzia miaka 05-14, kwani umri wa miaka 05, ni umri wa mtoto kuwa kwenye mpango wa chanjo za clinic na umri wa miaka 14 inasadikiwa kuwa umri wa mtoto ambaye bado kupevuka, utakaomwezesha kutambua athari ya kuwa katika Mazingira hatarishi ya maambukizi ya magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo.
Aidha amefafanua kuwa kampeni hii ni mwendelezo wa tatu kufanyika wakishirikiana na Wizara ya Afya kitengo cha magonjwa yasiyopewa kipaumbele nchini Tanzânia, ambapo ya kwanza ilifanyika mwaka 2014, na ya pili mwaka 2016.
"Tunategemea kutoa dawa kwa ajili ya kukinga magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa wanafunzi wa shule za msingi 157, zilizosajiliwa Manispaa ya Kinondoni, kuanzia wanafunzi wenye umri wa miaka 05 hadi miaka 14, hii itakuwa ni mwendelezo wa tatu kwa kampeni hii kufanyika." Amebainisha Dr. Neema.
Naye Bi Agnes Mgaya ambaye ni mratibu wa wauguzi Manispaa hiyo, katika mada yake ameyataja magonjwa yasiyopewa kipaumbele nchini Tanzania kuwa ni Trachoma, Usubi, Kichocho, minyoo ya tumbo, matende, mabusha na Ngiri maji.
Ameongeza kuwa magonjwa haya huambukizwa kwa njia tofauti tofauti, ambazo mwanadamu yeyote anaweza kujikinga nazo chache zikiwa ni kutumia chandarua, kumeza dawa za kujikinga na magonjwa hayo, na kufanya uchunguzi wa mara kwa mara.
Akitoa ufafanuzi wa matumizi ya dawa hizo Bi Sophia Mwilongo ambaye ni Mfamasia wa Manispaa hiyo, amethibitisha dawa hizo kutokuwa na madhara yeyote zikimezwa kwa utaratibu na Maelekezo ya mtaalam, na kuwataka wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kupewa dawa hizo, kwani ni kinga kwa magonjwa hayo ya kichocho na minyoo ya tumbo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.