Ni kauli yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe alipofanya ziara ya ukaguzi wa maeneo yaliyoainishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuwapanga wamachinga.
Amesema lengo la kutembelea maeneo hayo ni kujiridhisha na uhalali wake lakini pia ni kubainisha changamoto zilizopo ili ziweze kutatuliwa na wamachinga waweze kufanya biashara zao kwa utulivu na amani.
Amesema "Ndugu zangu wamachinga, njooni maeneo mliyopangiwa, nilazima mtambue Serikali inawajali sana. Lengo la Serikali ni kuhakikisha wenzetu hawa wanatafutiwa maeneo kwa ajili ya kufanya biashara zao, na ni lazima tujiridhishe maeneo hayo ni salama na inayo miundombinu inayokidhi kwa eneo hilo kuwa la biashara kama vile umeme, maji, choo, na barabara". Amefafanua Mhe. Gondwe.
Aidha amezitaka Taasisi husika kama TANESCO, DAWASCO na TARURA kuhakikisha wanashirikiana na Halmashauri kuboresha miundombinu ya msingi katika maeneo yaliyoainishwa ili yaweze kutumiwa na wafanyabiashara hawa katika utaratibu unaoeleweka na bila kupata bugudha yoyote
Akizingumza kwa niaba ya Dawati la kuwapanga wamachinga Wilaya ya Kinondoni, Mwenyekiti wa dawati hilo Bi. Leah Momba amesema vipo vigezo vinavyozingatiwa katika kuainisha maeneo ikiwemo eneo liwe la wazi, eneo kutokuwa na mgogoro wowote, eneo linalofikika na uwepo wa miundombinu ya maji, umeme na choo.
Katika hatua nyingine Mhe.Gondwe amelitaka Dawati la kuwapanga wafanyabiashara kuwa makini na kuzingatia haki katika upangaji wa wamachinga kwenye maeneo yaliyoainishwa kwani changamoto kubwa hutokea pale wanapopangiwa nafasi wasiokuwa wamachinga.
Maeneo yaliyotembelewa katika ziara hiyo iliyohusisha Kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya, Dawati la kuwapanga wamachinga Wilaya, Wakuu wa Idara na Vitengo ni eneo la Benaco lililopo Salasala, eneo la Kisanga pamoja na eneo la Ununio.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.