Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule ametoa siku 14 kwa wakazi wa Mtaa wa Kijijini Kata ya Kawe waliojenga karibu na barabara kuondoka mara moja.
Mhe. Saad amesema hayo leo Novemba 02, 2023 katika kikao kazi na Wananchi wa Mtaa huo wa Kijijini akiwa na lengo la kusikiliza kero zao pamoja na kukemea ukatili wa kijinsia katika maeneo hayo.
"Kutokana na kushamiri kwa vitendo vya unyasasaji wa kijinsia katika Mtaa wa Kijijini ambao unasababishwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa vibanda vya makazi katika eneo la barabara na lisilo rasmi kwa makazi hivyo natoa siku 14 kuondoa vibanda vyote ambavyo vimekuwa sababu ya uharifu na unyanyasaji wa kijinsia katika Mtaa huo," amesema Mhe. Saad.
Mbali na hayo pia Mhe. Saad amekemea vikali unywaji wa pombe kupitiliza kwani kufanya hivyo ndio chanzo kikubwa cha uwepo wa biashara haramu kama vile biashara ya ngono.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.