Wazazi na walezi wametakiwa kuwalinda Watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyopelekea kuua ndoto za Watoto wengi. Rai hiyo imetolewa na Afisa elimu Kata ya Mzimuni Mwl. Jane Malongo Mei 22, 2024 alipokutana na Wananchi wa Kata hiyo katika Ofisi ya Kata ya mzimuni.
"Watoto wanafanyiwa ukatili sana wakiwa sehemu mbalimbali na sehemu ambayo imekuwa na matukio mengi sana ni majumbani" amesema Mwl. Malongo.
Aidha, Mwl. Malongo, amewasihi akinamama na Wazazi kwa ujumla kuwalinda watoto dhidi ya matukio mbalimbali ya ukatili kwa kuwa wao wana uwezo wa kujenga ukaribu na kuibua matukio hayo.
"Msiwaamini sana watu wa karibu mnaoishi nao hasa wanaume awe ni kaka, mjomba au mpangaji mwezako hivyo muwajibike katika kuimarisha ulinzi kwa watoto." Ameongeza Mwl. Malongo.
Kadhalika, Mwl. Malongo Amemshukuru sana Diwani wa kata ya Mzimuni kwa kuweka juhudi zake katika suala la elimu ikiwamo kujenga uzio wa shule zote 3 za kata ya Mzimuni kwani kumeimarisha ulinzi kwa watoto sambamba na kuepusha utoro kwa wanafunzi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.