Walimu Wakuu wa Shule Msingi za Serikali na za Binafsi wamepewa Wito wa Kuimarisha Elimu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa mbinu za kisasa zinazoendana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia .Hayo yalizungumzwa leo Mei 30, 2024 na Mkuza Mitaala wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Bwn. Nchahoruri Joel katika Semina ya Mafunzo kuhusiana na Mtaala Mpya iliyohusisha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Serikali na Binafsi zilizopo ndani ya Wilaya ya Kinondoni iliyofanyika katika Ukumbi wa Soko la Magomeni.
Akizungumza katika semina hiyo, Bwn. Nchahoruri alisisitiza umuhimu wa walimu kubadilika na kwenda sambamba na mabadiliko ya kiteknolojia yanayotokea ulimwenguni.
"Ni lazima walimu wakuu wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba Wanafunzi wanapata elimu bora ya TEHAMA ambayo itawasaidia katika soko la ajira na maisha yao ya baadaye na katika kuhakikisha hilo nitaomba hata runinga za kujifunzia katika shule zetu za masingi ziwe runinga za kisasa zinazoendana na maendeleo ya teknolojia," Bwn. Nchahoruri alisema.
Aidha, Bwn. Nchahoruri alitoa wito wa kuboresha stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa wanafunzi kwa kuzingatia ufundishaji kwa kutumia njia za kisasa ikiwemo kufundisha kwa kutumia runinga ili kurahisisha Wanafunzi kuelewa kwa uharaka na usahihi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.