Suluhisho hilo limekuja leo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo kuzuru eneo lenye bwawa na kushauri kufunguliwa kwa barabara ya muda katika mazungumzo yaliyohusisha wananchi wa mji mpya, wamiliki wa viwanja vilivyopakana na bwawa pamoja na wadau wa maendeleo .
Akizungumza na wakazi hao, Mhe. Chongolo amesema kufunguliwa kwa barabara ya muda kutawawezesha wakazi wa wazo mji mpya kufika majumbani kwao, lakini pia kutatoa nafasi ya eneo linalojaa maji kuboreshwa kwa kusambaza kifusi na kuchimba mitaro itakayoelekeza maji katika mkondo wake ili kuzuia athari za uharibifu wa barabara.
Amesema " Kwanza tuondoe hatari iliyo mbele yetu, miti ing'olewe ili kuandaa eneo la barabara ya watu kupita ili waweze kufika katika makazi yao, kupatikane kifusi cha kujaza eneo kuyaelekeza maji kufuata mkondo wake, mana suala lililoko hapa ni makubaliano tu, baina ya mwenye kiwanja kilichopakana na bwawa kutoa eneo kwa muda ili waweze kusambaza kifusi kwa ajili ya kupata barabara ya muda, wakati tukiendelea kupata suluhisho la kudumu. jukumu langu ni kuhakikisha wananchi wanapata Amani katika makazi yao" Amesema Chongolo.
Aidha amemtaka Bw.Gerald Lusula Mwenye kiwanja Na.392 na Bwana Andrew Peter Mwenye kiwanja namba 393 vyote vikiwa vimepakana na eneo lenye bwawa kutoa ushirikiano katika kuhakikisha suluhu ya pamoja inapatikana kwa kuruhusu kusambazwa kifusi kwenye ukingo wa viwanja ili kupatikana kwa barabara ya muda kwa wakazi wa mji mpya kufika majumbani kwao huku wakiangalia suluhu ya kudumu ya eneo hilo.
Katika hatua nyingine ameiagiza kampuni ya Mecco inayojenga barabara ya wazo kutumia scaveta pamoja na greda kusambaza kifusi kitakachotolewa na kiwanda cha wazo ikiwa ni pamoja na mifuko 20 ya cement pamoja na kalvati kwa ajili ya kuboreshwa eneo hilo la bwawa.
Awali akiainisha changamoto ya eneo hilo Mhandisi wa Tanroad Bi.Mariam Hassan amesema ni kutokana na kuzuiwa kwa mkondo huo wa maji hali iliyopelekea kutuama na kusababisha bwawa linaloendelea kukua na kuharibu barabara.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.