Hayo yamebainishwa leo na Mratibu wa ICHF Manispaa ya Kinondoni Bi.Joyce John, katika mdahalo wa afya ya uzazi kwa jamii, uliofanyika katika kituo cha afya cha Tandale.
Amesema suala la uzazi wa mpango ni suala mtambuka linalomtaka baba na mama kijadiliana kwani watoto wanaozaliwa wanahitaji elimu ili waweze kujikwamua kimaendeleo, kiuchumi, na kifikra kuelekea uchumi wa Kati wa viwanda.
"Tunahitaji watu au uzao wenye fikra yakinifu na uwezo wa kupambanua mambo kwa weledi ili kutoa ufumbuzi wa mahitaji ya jamii yetu, hata hivyo hayo yanawezekana ikiwa afya ya uzazi itazingatiwa ipasavyo maana ndiyo msingi imara wa jamii inayojitosheleza" Ameeleza Bi Joyce.
Akifafanua umuhimu wa afya ya uzazi kwa jamii Bi Fatma Juma Watanga ambaye pia ni muuguzi msaidizi wa kituo cha afya Tandale, amesema mtoto aliyenyonya ziwa la mama kwa miaka miwili mfululizo, anakuwa na afya njema ya akili, ikiwa ni pamoja na kusukuma gurudumu la maendeleo, tofauti na ambaye hakunyonya kwa muda huo.
Katika mdahalo huo pia umehudhuriwa na wananchi kutoka kata na mitaa ya tandale, pamoja na wauguzi kutoka kituo cha tandale, na kujadili nini maana ya afya ya uzazi, namna na njia za kufuata ili kuwa na afya ya uzazi na umhimu wake.
Aidha washiriki wa mdahalo huo pia wameushukuru uongozi kwa kuwapatia mada hizo zilizotoa mwanga wa nini kifanyike katika kurudisha upendo uliokuwa umepotea katika jamii.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.