WAJUMBE WA MABARAZA YA KATA MANISPAA YA KINONDONI WATAKIWA KUSIMAMIA SHERIA KATIKA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI.
Wajumbe wa Mabaraza ya Kata Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni pamoja na kutoa haki kwa Wananchi kuhusiana na masuala ya migogoro ya Ardhi yanapoletwa kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo jana alipokutana na wajumbe wa Mabaraza hayo kikao kilichokuwa na lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazo wakabili ambapo pamoja na mambo mengine amewakumbusha kutambua wajibu na majukumu yao.
Alisema katika kutambua wajibu wao ni vema wakajiepusha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwakuwa vinaweza kuharibu uaminifu waliopewa na Halmashauri pamoja na kusababisha migogoro kwa Wananchi.
Katika kikao hicho pia Mhe. Chongolo na wajumbe wa Mabaraza hayo wamejadili hatua zitakazo wawezesha kupunguza kama sio kumaliza kabisa migogoro katika Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto za wananchi na hivyo kuleta tija na ufanisi wa utendaji wa kazi zao.
Aidha amewataka wajumbe hao kuweka utaratibu wa kutembelea maeneo ambayo yanashukiwa kuwa na migogoro na kwamba kwakufanya hivyo itakua ni njia sawia katika kukabiliana na changamoto ambazo wananchi wanakutana nazo.
“Mabaraza haya yapokisheria, mnanguvu ya kuwachukulia hatua wale ambao wanakiuka sheria zilizoweka, kukaidi maelekezo mnayotoa, msiwe wanyonge fanyeni kazi kwakusimamia haki na sheria kama ambavyo siku zote Rais wetu Dk. John Pombe Joseph Magufuli anatuelekeza” alisema Mhe. Chongolo.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo ameipongeza Idara ya sheria ya Manispaa hiyo kwakufanyakazi bega kwa bega na Mabaraza hayo na hivyo kuleta mafanikio makubwa ya utatuzi wa migogoro ya Ardhi.
Wajumbe wa Mabaraza ya Kata wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mhe. Daniel Chongolo.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha habari na Mahusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.