Wahudumu wa Afya katika Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kufanya kazi kwa moyo ili kupunguza changamoto ndogondogo katika Vituo vya Afya.Wito huo umetolewa Februari 21, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kinondoni wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.6.
Akiongea katika ziara hiyo Mhe. Chalamila amesema kuwa ujenzi wa Kituo hicho utaenda kupunguza adha na changamoto walizokuwa wakipata wakazi wa Kata ya Kinondoni kwani hapo awali hapakuwa na Kituo wala Zahati ya kutolea huduma za kiafya ndani ya Kata hiyo.
"Kutokana na kasi nzuri ya ujenzi huu unavyokwenda huku ukizingatia ubora wa hali ya juu hivyo niwaombe wahudumu wa afya ndani ya Manispaa ya Kinondoni kufanya kazi kwa moyo ili kupunguza changamoto ndogondogo zinazojitokeza katika vituo vya afya na Zahanati zetu kwani Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa pesa nyingi kutekeleza moradi hii ya afya," amesema Mhe. Chalamila.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.