NI KWA ZILE SHULE ZINAZOZUNGUKA MAENEO YA KARIBU NA VITU HIVYO ILI NAO WAWE MABALOZI KWA WANAFUNZI WA SHULE NYINGINE.
Agizo hilo limekuja mara baada ya Kamati ya kudhibiti UKIMWI Kinondoni, kutembelea shule za Msingi Bunju A na Kawe kwa lengo la kujiridhisha na uelewa wa wanafunzi hao juu ya masuala ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, na kubaini kuwa uelewa wao ni mkubwa tofauti na shule zisizopata fursa hiyo ya elimu.
Akifafanua zaidi kuhusu hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe George Manyama amesema kuwa kwakuwa wahudumu wa vituo vya Afya wanao utaalamu wa kutosha kwa maswala haya ni vema wakatumia kila mbinu waijuayo kuhakikisha watoto wetu wanapata elimu ya kutosha kwa kuwa wataalam hawa wa zahanati na vituo vya afya wanao mchango mkubwa na mbinu mbadala katika kufikisha ujumbe wa masuala ya elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa wanafunzi hivyo waitumie.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la kawe ambae pia ni mjumbe wa Kamati hiyo Mhe Halima Mdee amewataka wanafunzi hao kujitambua na kuishi utoto wao huku akiwakanya kuacha kuanza kufanya Mambo ya wakubwa wakiwa Katika umri mdogo.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.