Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo alipozuru katika soko hilo na kukagua hali ya miundombinu na uchakavu wa vizimba, pamoja na kuzungumnza na wafanyabiashara hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika sokoni hapo.
Amesema lengo la Serikali ni kuboresha maeneo ya masoko pamoja na wafanyabiashara wake ikiwa ni mpango mkakati wa kuziboresha Halmashauri zake, kwa kuziwezesha kutekeleza miradi ya kimkakati inayoweza kuwaingizia kipato na soko la Magomeni kuwa sehemu ya mpango huo.
"Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ameamua kufanya uwezeshaji maalum kwa baadhi ya miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri, hivyo zimetengwa Tsh bilioni 146, kutekeleza miradi 22 nchi nzima, ambapo bilioni 53.7 zinaenda kwenye masoko na 67.3 zinaenda kwenye stendi za mabasi". Ameinisha Jafo.
Mhe. Jafo amesema kwa Serikali kutenga bilioni 9 ni neema kwa wafanyabiashara soko la Magomeni, na kumtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kusimamia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Naye Afisa Masoko wa Manispaa hiyo Bw. Zahoro Haruna akitoa taarifa ya soko hilo kwa Mhe. Waziri amesema miundombinu ya soko hilo ni mibovu na kufanya wafanyabiashara zaidi ya mia sita (600) kuwa na mazingira magumu katika maeneo yao.
Ameongeza kuwa kwa kuboreshwa soko hilo pia kutachangia ongezeko la pato la Halmashauri kwani kwa sasa kiasi kinachokusanywa ni takriban Tsh. milioni moja na laki mbili kwa mwaka, ambapo kukamilika kwake kutawezesha magari 150, kuegeshwa kwa pamoja na kodi kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni 500 kukusanywa kwa mwaka.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.