Hayo yamebainika leo wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Daniel Chongolo kwa kushirikiana na asas ya Human releif foundation walipozuru katika kituo cha watoto yatima cha Kijiji cha Furaha kilichopo Mbweni na kutoa msaada wa sukari, unga, mafuta ya kupikia na mchele kwa kituo hicho.
Amesema ni jukumu letu kuhakikisha watoto hawa wanapatiwa upendo unaostahili ikiwemo haki za kisheria za watoto ambazo ni kulindwa, kusikilizwa, kupatiwa elimu, makazi na malazi.
Amesema "Watoto hawa ni jukumu letu sote, lazima tuwapende na kuwajali, kwani jamii yetu imezungukwa na watu mbalimbali wanaohitaji kutazamwa kwa jicho la tatu kama vile watoto yatima na wengineo, hivyo ni wajibu wetu kuwapatia vitu wanavyohitaji".Mhe. Chongolo
Ameongeza kuwa kilichofanywa leo na Mr Mbarak F.Baghumesh kutoka asas ya Human Releif Foundation ni ishara kubwa ya upendo na inatakiwa kuigwa na kila mtu, kwani hata yeye hajaangalia dini yake isipokuwa ametanguliza upendo na uthamani wa kiutu.
Aidha ameahidi kushirikiana bega kwa bega na wadau wengine katika kuhakikisha changamoto mbalimbali zinazoikabiri taasisi ya Kijji cha Furaha zinatatuliwa na kuwataka watu wa idara ya ustawi wa jamii Manispaa ya Kinondoni kutafuta njia mbadala za kuwasaidia watoto yatima wanaomaliza shule katika vituo mbalimbali.
Kwa upande wake Mr Mbarak ambaye ni Operation Manager wa shirika la Human Relief Foundation, amesema kuwa mbali na kutoa msaada hui, ataendelea kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya katika kuwathamini watu wenye mahitaji maalum bila kujali rangi wala dini zao.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.