Hayo yamezungumzwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa kituo cha polisi cha mbweni kilichojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na wadau wa maendeleo pamoja jeshi la polisi kilichopo Manispaa ya Kinondoni.
Amesema ujenzi wa vituo hivi utawarahisishia polisi wetu kufanya kazi katika mazingira rafiki na salama hasa ikizingatiwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ipo makini katika kuhakikisha wanaimarisha miundombinu katika jeshi.
"Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina nia madhubuti ya kuhakikisha vituo hivi vya polisi vinaboreshwa, na ndio maana Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli ameridhia kutumika kwa Bilioni Kumi kwaajili ya ujenzi wa nyumba za maaskari polisi, na kutoa kibali cha ajira kwa Askari 1500 ,"Amebainisha Waziri Majaliwa
Aidha amewataka jeshi la polisi pamoja na maboresho hayo, kuenda sambamba na uimarishaji wa nidhamu na maadili ya jeshi hilo.
Awali akiongea kabla ya kumkaribisha waziri mkuu, Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mh Hamad Masauni amesema kituo hicho ni msaada mkubwa kwa wananchi wa mbweni na maeneo ya karibu kwani pamoja na mambo mengine kutakuwa na dawati la jinsia litakaloshughulikia kero mbalimbali za wananchi.
Naye Kamanda wa jeshi la polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro amewataka wafungwa waliopata msamaha wa Rais kuwa raia wema,kujiepusha na uhalifu ili kuondokana na makosa yasiyoyalazima kwani kwa kutokufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika ziara yake hiyo, Mh Waziri Majaliwa amezindua kituo cha polisi Mburahati na Kiluvya vilivyopo Manispaa ya Ubungo katika hafla iliyoambatana na ugawaji wa vyeti kwa wadau mbalimbali walioshiriki ujenzi wa vituo hivyo ambao ni kampuni ya Estim, Twiga cement, TRA, Bakhresa,pamoja na Lake oil.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.