Wakati Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ikiendelea na oparesheni ya kubaini, kuvunja na kuteketeza madanguro, baadhi ya wanawake wanaofanya biashara haramu ya miili yao wamejitokeza kuomba msaada ili wapate shughuli halali.
Hayo yamebainishwa leo Kata ya Tandale eneo la Uwanja wa Fisi baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Saad Mtambule, akiambatana na Mstahiki Meya, Mheshimiwa Songoro Mnyonge, kufika eneo hilo kwa lengo la kukagua ubomoaji wa madanguro hayo takribani 350.
"Mimi ni mama wa familia wa watoto wanne wanaonitegemea, hivyo binafsi yangu ninaomba msaada kutoka kwako Mstahiki Meya na Manispaa iniangalie kwa jicho la huruma ili niweze kuendesha familia yangu", alisema.
Aidha, Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Mtambule alisema, "tayari kama Manispaa imeanza mchakato wa kuwatambua wale wote waliokuwa wakifanya biashara hiyo ili waweze kupata mkopo wa asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.