Hayo yamezungumnzwa leo na Katibu Mkuu Tume ya Utumishi wa waalimu Bi Winifrida Rutahindura katika mkutano wake na waalimu wakuu, wakuu wa shule, pamoja na waratibu wa Elimu uliofanyika oysterbay shule ya Msingi Manispaa ya Kinondoni.
Amesema lengo la Mkutano wake huo ni kukumbushana majukumu ya kazi katika utendaji, maadili ya kazi, pamoja na maswala yanayohusiana na ajira, nidhamu, na sheria ndogo za kazi zinazompasa mwalimu kuzizingatia.
Ameongeza kuwa kazi ya usimamizi wa maadili ya kazi ya ualimu ni jukumu la kila mmoja, jamii, waalimu wenyewe, viongozi katika shule, Kata na Wilaya, kwani Mwalimu anao wajibu mkubwa wa kumlea mtoto, kusimamia kazi yake ya ualimu, na kuliendeleza Taifa.
"Kila mtu ajitume, kwa nafasi yake, waalimu fundisheni kwa kutumia text books na sio mitihani, nafasi mliyonayo kwa Jamii na kwa Taifa ni kubwa Sana, hivyo zingatieni maadili na uwajibikaji katika kazi yenu hii "amesisitiza Katibu
Naye Mkurugenzi wa ajira na Maendeleo ya watumishi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bi. Christina Hape alipokuwa akizungumnzia maswala ya kupandishwa madaraja ameainisha vigezo vyake kuwa ni Bajeti, Ikama, Tange, utendaji kazi wa mtu, pamoja na muundo.
Aidha ameainisha hatua zinazotakiwa kuchukuliwa kwa mwalimu aliyekosea kuwa ni kupatiwa hati ya mashtaka inayoelezea kosa lake na kupewa muda wa kujitetea.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo aliainisha majukumu ya tume ya Utumishi wa waalimu yanayotakiwa kuzingatiwa kuwa ni kushughulikia maswala yahusuyo ajira, Mafao ya wastaafu, kusimamia maadili na nidhamu, kusimamia program za mafunzo, kuandaa kanzidata pamoja na kufanya tathmini ya hali ya waalimu ikiwa ni pamoja na kumshauri Waziri mwenye dhamana maswala mbalimbali ya sekta hiyo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.