KUKUBALIWA kwa ombi la Vyama vya Siasa Wilaya ya Kinondoni kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa limepokelewa kwa furaha.
Furaha hiyo imefuatia ombi hilo kuungwa mkono na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songoro Mnyonge. Ombi hilo liliwasilishwa na Mwenyekiti wa Wilaya wa Chama cha Demokrasia Makini, Mheshimiwa Costa Kibonde katika kikao cha Baraza la Ushauri la Wilaya lililoketi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya Manispaa kwa mwaka 2024/2025.
Mheshimiwa Mnyonge alisema, "naunga mkono Vyama vya Siasa kutembelea miradi ya maendeleo. Badala ya sisi kuwa wasemaji wa miradi hiyo, wenzetu pia wakiona watatusaidia kutusemea."
Awali Mheshimiwa Kibonde alieleza kuwa, "Manispaa mnatekeleza miradi vizuri sana, tunaomba na sisi tupate nafasi ya kwenda kuitembelea ili tuweze kuyazungumzia mazuri yanayotekelezwa na Serikali hii."
Kadhalika Mheshimiwa Mnyonge aliwaomba viongozi hao wa vyama vya Siasa kuwa Mabalozi wazuri wa kuyazungumzia mafanikio ya utekelezaji miradi ya maendeleo chini ya Serikali ya awamu ya sita.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.