Imeelezwa kuwa matone ya Vitamini 'A' kwa watoto husaidia kukinga tatizo la vipele vya ngozi kwa watoto chini ya umri wa miaka Mitano.
Hayo yamebainishwa Desemba 18, 2023 na Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Magomeni, Bi. Luwiza Masanyila, wakati akitoa wito kwa Wazazi kuwapeleka Watoto kupata Matone ya Vitamini 'A'.
Alisema "kuna ongezeko kubwa la watoto wenye shida ya ngozi(vipele), " na kutoa rai kuwa, "wazazi wajitahidi kuwapeleka watoto katika Vituo vya Afya kwa ajili ya kupata matone ya Vitamini A kwa ajili ya kupata kinga."
Manispaa ya Kinondoni ilianza zoezi la utoaji Matone hayo Disemba Mosi, 2023 na inatarajia kukamilisha zoezi hilo Januari 5, 2024, ambapo huduma hiyo itatolewa katika vituo vyote vya huduma za Afya vya Serikali na binafsi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.