Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Daniel Chongolo, alipokuwa mgeni rasmi katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi oysterbay, ikihusisha wajasiriamali kutoka kata zote 20, kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika maswala ya mikopo na fursa zilizopo.
Amesema mafunzo haya na mikopo hii iliyo na riba nafuu, ikawe chachu ya kujishughulisha kwani ndio msingi madhubuti wa maendeleo kwa vijana hasa ikizingatiwa Serikali ya awamu ya tano, imelenga kuimarisha uchumi wa vijana na kinamama kwa kujishughulisha na ujasiriamali.
"Sitegemei wala sitaki kuletewa kesi za mtu kutaka kuuziwa vitu vyake kwa sababu ya kumdhamini mtu mwingine au kwa kushindwa kurejesha mikopo na wakati serikali imetoa mikopo kwa vijana na wajasiriamali tena bila riba" amefafanua Mhe Chongolo.
Akizungumnzia mafunzo hayo Mkurugenzi kutoka TAEDO ndg Kenan Kihongozi amesema semina hii ni madhubuti kwa ajili ya vijana na hata mada zilizoandaliwa ni mahususi kuziendea fursa hasa za kiuchumi, kwani mikopo bila elimu kwaweza kuwa kikwazo cha kujikwamua na fursa hizo.
Amezitaja mada zilizofundishwa katika semina hiyo kuwa ni jinsi ya kufanya ufugaji bora wa kuku, utengenezaji wa sabuni za unga, maji na vipande, jiki, mbegu za vitunguu, mbolea ya maji na utengenezaji wa sabuni au dawa za kusafishia sakafu na marumaru.
Katika hatua nyingine, wajasiriamali hao wameishukuru Serikali kwa kuwapa mikopo, hali inayotoa hamasa kwao ya kutafuta vitegauchumi mbalimbali kupitia hiyo mikopo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kindoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.