Hayo yamejidhihirisha pale ambapo kiwanda cha wazo kimefanikiwa kujenga daraja litakalowaunganisha wananchi wa pande mbili za mtaani hapo waliokuwa wakishindwa kuziendea shughuli zao kutokana na ubovu wa barabara uliokuwepo hapo awali.
Daraja hilo lililozinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ali Hapi katika ziara yake ya kikazi limekuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wakaazi wa eneo hilo watembea kwa miguu na watumiaji wa vyombo vya moto, kwani hapo awali walipata adha ya kushindwa kupita kutokana na uharibu na ubovu wa barabara hiyo hasa nyakati za mvua.
Akizindua daraja hili Mh Hapi amesema "Huu ndio uzalendo tunaoutaka, kwani Serikali ni pamoja na ninyi wananchi, sasa kwa kufanya hivi mmeonesha uwajibikaji na uzalendo mkubwa uliotukuka utakaosaidia wananchi kupata huduma muhimu kwa kupita wakiwa wanaenda kwenye shughuli zao za ujenzi wa Taifa, kuelekea uchumi wa kati wa viwanda " Amesema Hapi.
Kadhalika katika ziara yake hiyo pia amefanikiwa kuweka jiwe la msingi ofisi ya Serikali ya mtaa wa Kisanga, Nyakasangwe, pamoja na shule ya Sekondari mivumoni, na kutembelea shule ya Msingi salasala, ujenzi wa choo cha wafanyabiashara wazo, ujenzi wa kituo kidogo cha polisi Salasala, na Bustani ya mfano katika ofisi ya Kata ya Wazo.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya, amezitaka mamlaka husika na maswala ya Mazingira kuhakikisha wanaishughulikia kwa ukaribu na haraka changamoto ya mmomonyoko wa ardhi katika shule ya Msingi salasala unaotishia kubomoa shule hiyo.
Hii ni Kata ya tatu kutembelea, katika ziara yake hiyo ya kikazi yenye lengo la kutembelea kata zote 20,za Manispaa ya Kinondoni kuangalia utekelezaji wa shughuli za Serikali, na kufanya Mikutano ya hadhara na wananchi wa kata hizo.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.