Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imezindua rasmi utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa kutumia hereni za kielekitroniki katika mtaa wa Ada Estate, Kata ya Kinondoni leo Jumatatu Septembea 26, 2022.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mwajuma Chaurembo aliwaambia wafugaji na wadau wengine waliohudhuria katika uzinduzi huo kuwa mfumo huo wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji una manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kurahisisha biashara ya mifugo na mazao yake, mifugo kutambulika ilipo na wamiliki wake, udhibiti wa wizi wa mifugo, kurahisisha upatikanaji wa mifugo iliyopotea, kurahisisha upatikanaji wa mikopo na bima ya mifugo, kukabili magonjwa ya mlipuko, hakikisho la usalama wa chakula na kurahisisha uboreshaji wa koosafu za mifugo.
Naye Bertilla Lymo Mkuu wa Sehemu ya Mifugo aliwambia wadau wote waliohudhuria kuwa zoezi hili ni urejelezwaji wa mwongozo uliotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi juu ya urejelezwaji wa Sheria ya utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na.12 ya mwaka 2010 na Kanuni zake za mwaka 2011, Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Mifugo ya mwaka 2006 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lbara ya 40 ya mwaka 2020- 2025.
Akizungumzia lengo kuu la zoezi hilo alisema kuwa ni kuweka utaratibu mzuri wa kuwezesha utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo kwa kuonesha mahitaji, majukumu na wajibu wa kila mdau ili kufikia lengo la jumla la la mifugo yote ya Tanzania kutambuliwa na kusajiliwa.
Uwekaji huu wa alama za utambuzi kwa kutumia hereni unafanywa kwa ushiriano wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Sekta binafsi ambapo hereni bora za kielekitroniki zimeandaliwa na katika Manispaa ya Kinondoni litahusisha Kata zote 20 za Manispaa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serkalini: Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.