Wananchi wametakiwa kuendelea kufanya usafi kila siku ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko yanayotokana na uchafu.
Afisa Afya wa Kata ya Ndugumbi, Bi. Irene Sayo, aliyasema hayo Februari 24, 2024 katika zoezi la usafi lililofanyika katika Mtaa wa Kondoa uliopo Kata ya Ndugumbi.
Alisema, "Nawaomba Wananchi kuzoea kufanya usafi kila siku kwani usafi ni Afya na uchafu huzalisha magojwa."
Kwa mujibu wa Afisa Afya huyo, Kata hiyo inafanya vizuri katika utunzaji wa usafi tofauti na siku za nyuma.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.