Ufugaji wa mbuzi wa maziwa ni teknolojia inayovutia watu wengi katika banda la Manispaa ya Kinondoni katika maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere mkoani Morogoro.
Akizungumza katika maonesho hayo Bi. Catherine Makabwa amesema, ufugaji wa mbuzi wa maziwa umempa fursa ya kushiriki maonesho ya Nane Nane kupitia banda la Manispaa ya Kinondoni.
"Manispaa ya Kinondoni imenikutanisha na wajasiriamali, nimepata elimu ya kutosha, nimepata wateja, mapokeo ya bidhaa za mbuzi yamekua makubwa", amesema Bi. Catherine.
Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo soko litapanuka, kampuni itakua na anategemea kupata mrejesho kuhusiana na bidhaa za mbuzi ili aweze kukua zaidi kibiashara.
Aidha, Bi. Catherine ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo amejifunza ukarimu, upendo, ushirikano kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. "Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni unatoa mafunzo ya kutosha na kutamani kila mjasiriamali afanikiwe kibiashara".
Kauli mbiu ya maonesho ya Wakulima (Nane Nane) 2023 ni "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini: Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.