Hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi Kate S. Kamba alipofanya ziara katika Wilaya hiyo ,kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani katika miradi inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Amesema kwa hatua na ubora wa miradi hiyo, Kinondoni yadhihirisha ufuatiliaji, usimamiaji pamoja na mshikamano wa viongozi, walionao katika kuhakikisha wanafanikisha kusudi liletalo tija kwa wananchi wake.
"Nawapongeza Mh Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Baraza la madiwani, na wakuu wa idara na vitengo, hapa inaonesha kunamshikamano "
Ameongeza kuwa mipango na mikakati iliyowekwa ni vema ikatekelezwa ili wananchi waweze kunufaishwa nayo, hasa ikizingatiwa mikakati hiyo ipo katika ilani inayotekelezwa kwa mwaka 2015-2020.
Akisoma mpango wa utekelezaji wa Ilani ya CCM bi Gifti Isaya ambaye ni katibu tawala wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, amesema mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia maelezo yaliyopo kwenye ilani pamoja na sera na miongozo mbalimbali ya kisekta ikiwa ni pamoja na taarifa mbalimbali zinazokusanywa.
Aidha ameitaja mikakati hiyo kuwa ni uboreshaji na upanuzi wa huduma bora kwa jamii, uboreshaji wa elimu ya awali, msingi na sekondari, uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma kwa wananchi pamoja na uhamasishaji wa matumizi endelevu ya maliasili na ardhi.
Nyingine ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kodi, uimarishaji wa sekta zisizo rasmi, usimamizi wa usafi pamoja na kusimamia mikakati ya kupunguza maambukizi ya ukimwi.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg Aron Kagurumjuli ameishukuru kamati hiyo kwa kuitembelea Halmashauri na kukagua miradi inayotekelezwa na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na mapendekezo yaliyoinishwa na wajumbe.
Miradi iliyotembelewa ni ile ihusuyo sekta ya Elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.