Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila amewataka Wananchi wa Kata ya Makumbusho na Dar es Salaam kwa ujumla kutokuhusisha TANESCO na siasa.
Mheshimiwa Chalamila aliyasema hayo Februari 21, 2024 katika Mkutano wa hadhara uliofanya katika Viwanja vya CCM Mwinjuma Kata ya Mwananyamala.
"Hakuna kiongozi anayehujumu jitihada za Wananchi wake, hivyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan imejipanga kikamilifu kuondokana na changamoto hii kwani wametenga fedha kwa ajili ya ushirikiano na Uganda utakaozalisha Megawatt 14 lakini pia kukamilisha Bwawa la Nyerere ambapo kufika March 30, 2024 kero hii itakua imetatuliwa"
Aidha, Mheshimiwa Chalamila aliwataka Wananchi kuendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.