Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kupitia Divisheni ya Lishe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Rikolto na watoa huduma ngazi ya jamii (CHW) waendelea kutoa elimu juu ya ulaji wa mbaazi kwa watoto.
Elimu hiyo imetolewa katika Kata ya Kijitonyama ikiwa ni siku ya lishe ya robo ya kwanza ya mwaka 2023/2024 ikiwa na lengo la kuelezea umuhimu wa ulaji wa zao la mbaazi ikiwepo kuweka sawa presha ya mwili kuimarisha kinga ya mwili kutokana na uwepo wa Vitamin C.
“Ulaji wa mbaazi husaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha kinga ya mwili kwani ina virutubisho vingi sana kutokana na uwepo wa vitamin C kwa wingi hivyo jamii ione umuhimu wa utumiaji wa mbaazi kwa wingi hasa kwa watoto wetu,” amesema Bi. Anna.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.