Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, ameshauri ukaguzi kufanyika kila wakati ili kuzuia hoja zinazoweza kujitokeza.
Ushauri huo ameutoa leo katika Mkutano wa Baraza Maalum la Madiwani lililokutana kwa ajili ya kupitisha taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022.
"Ukaguzi uwe wa mara kwa mara, tusimsubiri CAG hadi aje, maoni ya Mkaguzi wa Ndani yafanyiwe kazi kwa umakini", alisema. Aliongeza kuwa, "tufanye kazi kuhakikisha tunazuia hoja za ukaguzi."
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Chalamila ameipongeza Manispaa ya Kinondoni kwa juhudi zake za ukusanyaji mapato ya ndani.
Pongezi hizo amezitoa baada ya Mweka Hazina wa Manispaa, Bwana Onesmo Mwonga, kueleza kuwa hadi sasa Manispaa imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 19 zikiwa ni ushuru wa wa Huduma (Service Levy) kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 20, 2023.
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kanzidata yetu ina walipa ushuru wa huduma 26,743 ambao hadi tarehe ya jana kiasi cha Shilingi Bilioni 19 zimekusanywa," alisema Bwana Mwonga.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.