Wakati maonesho ya wakulima (Nane Nane) Kanda ya Mashariki yakiendelea katika Viwanja vya J.K Nyerere mkoani Morogoro, Manispaa ya Kinondoni inajivunia kuwa na wajasiriamali wanaojihusisha na ufugaji wa kuku.
Akizungumza katika maonesho hayo mmoja wa wajasiriamali wanaojihusisha na ufugaji wa kuku Bi. Esther Ngamilo, "amesema kupitia maonesho haya amefaidika kwa kiasi kikubwa kwani amewahi kuwa mshindi wa ufugaji katika maonesho haya kupitia Wilaya ya Kinondoni".
Mbali na ushindi huo kutoka maonesho hayo ya Nane Nane pia Bi. Esther ameongeza kuwa mwaka uliofuata alifanikiwa kushinda kimkoa akiwakilisha ufugaji katika mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha, Bi. Esther ameongeza kuwa, ushindi huo umempa mafanikio makubwa sana ikiwemo kujulikana, kupata masoko katika supermarket na pia ameweza kupata fursa ya kufundisha wajasiriamali kuhusiana na ufugaji.
Nae mfugaji wa kuku chotara, Bw. Samuel Saimon amesema kushiriki maonesho ya Nane Nane kumempa wigo mpana katika sekta ya mifugo kwa kujifunza mambo mengi ya ujasiriamali.
Vilevile, Mustafa Ismail anasema maonesho haya yamempa mafanikio makubwa ikwemo kujulikana na kuendesha familia kupitia ufugaji.
Aidha, wajasiriamali hao wamefurahishwa na teknolojia mpya ya ufugaji wa mbuzi wa maziwa na bidhaa zitokanazo na maziwa ya mbuzi ambayo inaonekana kuwa ni teknolojia ngeni kwa wadau wengi.
Kauli mbiu ya maonesho hayo mwaka huu ni "Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula".
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.