Ubalozi wa Japan nchini, umeridhia kutoa msaada wa ujenzi wa matundu ya vyoo 34 katika shule ya Sekondari Mzimuni iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainika katika taarifa ya Kamati ya Huduma ya Uchumi, Afya na Elimu ya robo ya tatu iliyowasilishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne la Manispaa ya Kinondoni lililoketi Agosti 24, 2022.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa shule ya Sekondari Mzimuni ndiyo itakayo nufaika na msaada huo.
Aidha, Manispaa ya Kinondoni imetenga kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 84 kwa ajili ya ujenzi wa matundu 39 ya vyoo katika Shule za Sekondari.
Shule zitakazojengewa matundu hayo pamoja na idadi ya matundu kwenye mabano ni Boko (13), Twiga (13) na Mivumoni (13).
Aidha katika taarifa hiyo imeagizwa kufanyika ufuatiliaji wa haraka wa upatikanaji wa hati miliki za maeneo ya shule za sekondari na msingi.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.