NI KUFUATIA SEMINA ELEKEZI ILIYOTOLEWA KWA WATUMISHI AJIRA MPYA MANISPAA YA KINONDONI.
Uadilifu, uwajibikaji na uzalendo vyatajwa kuwa nguzo muhimu ya utendaji wa kazi katika Utumishi wa Umma, utakaoleta matokeo chanya katika kutoa huduma bora kwa mwananchi, ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu za utekelezaji wa majukumu kwa wakati na weledi.
Hayo yamebainishwa leo na Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Kinondoni Bi. Fauzia Nombo, alipokuwa akifungua semina elekezi ya siku moja kwa watumishi ajira mpya sekta ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ugavi na Uhasibu, iliyofanyika katika ukumbi mdogo Manispaa ya Kinondoni.
Amesema, ajira mpya lazima watambue umuhimu wa nafasi waliyoipata ya utendaji katika Utumishi wa umma, na kuhakikisha wanaitendea haki kwa kuwatumikia wananchi na kutoa huduma bora kwa wakati.
"Jamani ni lazima muelewe katika Utumishi wa Umma, kinachohitajika ni uwajibikaji na weledi, lakini pia matumizi sahihi ya lugha za uadilifu kwa wateja zitumike, kadhalika charting wakati wa kutoa huduma usiwepo, ili tuweze kutoa huduma bora kwa wananchi wenye uhitaji wa huduma hiyo. "Amesisitiza Bi. Fauzia.
Aidha ameainisha mada zitakazofundishwa kwenye semina hiyo kuwa ni haki za Mtumishi wa Umma, kanuni na maadili ya Utumishi, Mafunzo ya ujazaji wa Opras, Uandaaji wa mipango ya Maendeleo katika Serikali za Mitaa, na Umuhimu wa ushirika katika Maendeleo ya Kiuchumi na kijamii.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.