Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wameaswa kuzingatia misingi ya utumishi wa umma iliyopo kwenye hati ya kiapo kwa kuwa wazalendo wanapokuwa mahali pa kazi. Afisa Maadili Sekretarieti ya Maadili, Bw. Saidi Katani, alisema kuwa, "Mtumishi wa Umma aliyetukuka ni lazima awe mzalendo kwa vitendo kwa kufuata maelekezo yaliyopo ndani ya hati ya kiapo. Ili uwe mzalendo ni lazima kutekeleza majukumu bila kusukumwa."
Aidha, Bw. Katani aliwaasa Watumishi wa Umma kuzingatia msingi wa kutoa huduma bora kwa Umma wote pasipo kubagua watu.
"Mtumishi wa Umma unapaswa kuzingatia kutoa huduma bora na stahiki kwa watu wote pasipo kubagua mtu yeyote kulingana na dini, kabila au jinsia."
Bw. Katani aliyasema hayo wakati wa kikao kazi na Maafisa Afya, Ugani na Watendaji wa Mitaa kilichofanyika Mei 15, 2024 katika Ukumbi wa Soko la Magomeni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.