Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Taifa Bi. Fatuma Kange, amewataka wanawake wajasiriamali kutumia jukwaa la teknolojia kutangaza biashara zao ndani na nje ya Nchi.
Bi Fatuma Kange ameyasema hayo wakati wa ufungaji wa wiki ya majukwaa ya uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ngazi ya mitaa Wilaya ya Kinondoni, yaliyofanyika leo Novemba 24, 2023 katika viwanja vya Biafra.
Bi Fatuma Kange amesema kuwa biashara wanazofanya wanawake wajasiriamali zinaweza kufanyika kwa weledi mkubwa na mafanikio ikiwa watatumia Maendeleo ya teknolojia iliyopo. "Wanawake tutumie jukwaa la teknolojia kutafuta mtandao wa kuuza bidhaa zetu, tusitumie jukwaa hilo la teknolojia kupiga umbeya" ameongeza Bi. Fatuma Kange.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.