Hayo ni maneno yake Mstahiki Meya Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta, alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha wazazi takriban 720, wa wanafunzi wa Sekondari za Serikali wanaosoma mchepuo wa masomo ya Sayansi katika Sekondari 22, kati ya Sekondari 25, za Serikali za masomo hayo zilizopo Manispaa hiyo, kikao kilichofanyika katika shule ya Sekondari Turiani.
Amesema mwalimu na mzazi wanatakiwa kusimama kwa pamoja na kuzungumnza lugha moja itakayomweka mwanafunzi kwenye mstari uliosambamba utakaompelekea katika ufaulu wa masomo yake hayo ya Sayansi.
"Juhudi ya mwalimu pamoja na mzazi ndio itakayompeleka mtoto kwenye ufaulu mzuri, hivyo ewe mzazi, hakikisha unakuwa msimamizi wa kwanza wa mwanao, fuatilia maendeleo, kagua homework, wasiliana na Mwalimu akupe Maendeleo ya mtoto, hiyo ndio njia nzuri ya ushirikishwaji "Amesisitiza Meya.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini Rais Dr. John Pombe Magufuli imefanya makubwa kwenye sekta ya elimu ,ikiwa na lengo la kila mwanafunzi kupata haki sawa katika eneo hilo, hasa ikizingatiwa ni Serikali ya uchumi wa Kati wa viwanda, yenye uhitaji wa wahandisi wa kuendesha mitambo, na wataalam kwa uzalishaji wa bidhaa, ambapo wanafunzi wetu wa masomo hayo ya sayansi wapo kwenye nafasi kubwa ya kusimamia na kuendesha viwanda hivyo.
Naye Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa hiyo Ndg Rodgers Shemwelekwa alipokuwa akifafanua lengo la kikao hicho kwa Meya huyo amesema, pamoja na mambo mengine lakini kubwa ni kuwaelimisha wazazi kuwa na uelewa wa pamoja wa elimu msingi bila malipo na ulipaji wa kodi, wajibu wa wazazi katika kuwasimamia wanafunzi, na hali ya ufaulu wa mitihani ya Taifa, pamoja na mpango mkakati wa idara ya Elimu Sekondari wa kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu.
Mkutano huo umehusisha Afisa elimu taaluma, Afisa elimu takwimu na vifaa, bodi ya shule pamoja na wazazi takribani 720 wa wanafunzi kutoka shule za Sekondari ya Mbezi, Hananasifu, Kambangwa, Turiani ,Kigogo, Salma kikwete, Makumbusho na Makongo juu.
Wengine ni wazazi kutoka Sekondari ya Kawe ukwamani, Mikocheni, Twiga, Kisauke, Mbopo Maendeleo, Mtakuja,
Nkondo, Boko, Mabwe, Bunju A, na Mbweni teta.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.