Ni kauli yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala, alipozuru eneo la Coco-Beach na kuzungumza na wafanyabiashara wa eneo hilo katika kikao kazi kilichofanyika leo, kwa lengo la kutafuta namna bora ya uboreshaji wa fukwe hiyo bila kubugudhi wafanyabiashara hao kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amesema hatua hiyo ni katika kutekeleza mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuboresha maeneo ya fukwe ikiwa ni pamoja na kuzifanyia usafi hatua kwa hatua kwa lengo la kuongeza thamani ya eneo itakayoleta ubora unaokidhi hali itakayopelekea wananchi kupata mahali pa kuburudika.
Ameongeza kuwa mazingira ya fukwe yanapaswa kuwekewa mpango mkakati wa kuboreshwa ikiwa ni pamoja na kuwekewa miundombinu rafiki kwa matumizi ya wanadamu ikiwemo choo, umeme, maneneo ya kupumzika, maeneo ya biashara pamoja na mazingira safi.
"Hatuwezi kuwa na Beach ambazo ukikaa unaziba pua, moja ya tatizo la beach zetu za Dar es Salaam hazifanyiwi usafi una "suffocate", ni lazima fukwe hizi ziendelezwe na kufanyiwa usafi"
RC Makala.
Aidha amewataka wafanyabiashara wote wa eneo hilo kurekodiwa katika daftari maalumu huku wakitaja majina yao, namba za simu, Mtaa wanakotoka, biashara wanayofanya na namba ya kitambulisho cha NIDA au kupigia kura lengo likiwa ni kuwaweka katika utaratibu maalumu lakini pia ni sehemu ya kumbukumbu mara baada ya maboresho ya eneo hilo.
Kadhalika amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanaziweka fukwe pamoja na barabara za Halmashauri zao katika hali ya usafi.
Katika hatua nyingine amezitaka Taasisi mbalimbali ikiwemo Cocacola, na AZAM kufanya utafiti wa jinsi gani wanaweza kushirikiana pamoja na Serikali katika kuboresha fukwe hiyo kubwa likiwa ni kuyaweka mandhari yake katika ubora uliokubalika.
Kikao kazi hicho kimehusisha Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa Idara na Vitengo, Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, wadau wa maendeleo wakiwemo TBL, Bakhresa, Cocacola, Azam pamoja na wafanyabiashara wa eneo la Coco-Beach.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.