Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Jenista Mhagama (MB), amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia TEHAMA katika utendaji kazi wa kila siku.
Waziri Mhagama ameyasema hayo wakati akifunga kikako kazi cha tatu cha Serikali Mtandao. Kikao kazi hicho kilichoanza Februari 8, 2023 jijini Arusha kimehimitimishwa leo.
Amesema, "mnapotoka hapa mjitathmini kila mmoja, Kama Taasisi yako haijaanza kutumia TEHAMA, muende mkaanze kutumia".
Ameagiza vikao vyote vya Menejimenti na vya Mabaraza ya Madiwani kuendeshwa kimfumo; kuendelea kufanya upekuzi wa watumishi wote wa TEHAMA; kufanya kazi kwa weledi na uzalendo na kutumia mfumo wa e-mrejesho kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi.
Waziri Mhagama pia amekemea vitendo vinavyokwamisha ukusanyaji wa mapato kwa kisingizio cha mtandao kuwa chini.
Miongoni mwa maazimio hayo ni Taasisi zote kutumia TEHAMA; kuhuishwa kwa Tovuti; kusimamia Sheria, Kanuni na Miongozi ya Serikali Mtandao; vifaa vya TEHAMA kutengenezwa hapa nchini na uendelevu wa mifumo ya TEHAMA.
Ameagiza Mamlaka zote kutekeleza maazimio yote 12 ya Kikao kazi hicho na kuleta na kuomba kibali kabla ya utekelezaji wa miradi ya TEHAMA
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.