Wanufaika wa fedha kutoka Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) katika Wilaya ya Kinondoni wameaswa kutumia fedha hizo kuimarisha uchumi wao binafsi kwa kuanzisha vitegauchumi vitakavyowakwamua kwenye umaskini badala ya kutumia fedha hizo kwenye starehe.
Haya yalisemwa Mei 17, 2024 na Afisa Ufuatiliaji TASAF kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bi.Teddy Kyara katika zoezi la Uhakiki na Uboreshaji wa Taarifa wa daftari la TASAF kwa wanufaika katika linaloendelea katika Wilaya ya Kinondoni.
"Lengo la fedha za TASAF ni kuimarisha uchumi wa kaya Maskini hivyo hicho kidogo mnachokipata mjitahidi kukidunduliza na kuanzisha biashara mbalimbali.Msitumie fedha hizo kufanyia starehe badala yake tumieni fedha hizo kukuza uchumi wenu."
Aidha Afisa Muwezeshaji TASAF kutoka Kata ya Mzimuni Bi.Emelia Anyasisye amewaasa wanufaika wa fedha kutoka TASAF kuzingatia Afya zao kwa kufanya mazoezi ya kuimarisha mawili pamoja na kula mlo bora.
"Ni muhimu kufanya mazoezi,kula mlo bora na pia kupima Afya yako mara kwa mara kuimarisha afya zenu.Ambapo Kiafya inashauriwa kufanya mazoezi kwa dakika 30, kulala masaa 8, kunywa maji glasi 8 na pia muepuke kula vya kula vyenye sukari nyingi kwani husababisha magonjwa sugu ambayo ni hatari kwa afya."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.