Wazazi na Walimu katika Shule ya Msingi Ally Hassan Mwinyi iliyopo Wilaya ya Kinondoni wamepewa wito wa kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ili kuwakinga dhidi ya Saratani hiyo.
Wito huo ulitolewa Aprili 23, 2024 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Bi. Stella Msofe, kwenye uzinduzi wa Chanjo hiyo ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana wa umri wa miaka 9 mpaka miaka 14. Uzinduzi huo ulifanyika katika Shule ya Msingi Ally Hassan Mwinyi.
Bi. Msofe alisema, "Hii ni chanjo salama na haina madhara, hivyo kwa wale wazazi ambao hawajaruhusu watoto wao kupata chanjo wawaruhusu, pia walimu muwe mawakili wema wa kusambaza habari njema na kuwaelimisha wazazi kuhusiana na umuhimu wa chanjo ya saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana ."
Aliongeza kuwa, "Matibabu ya saratani yana gharama kubwa kuliko chanjo. Hivyo tunapongeza wazazi waliowaruhusu watoto wao kupatiwa chanjo kwasababu kupitia chanjo hii watoto watakuwa salama na wataweza kutimiza ndoto zao za kuwa wataalam mbalimbali katika nchi yetu."
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.