Ni kauli yake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda alipokuwa akiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa barabara ya Africana salalsala Kinzudi inayojengwa na TARURA, yenye urefu wa km 1.7, na baadae kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mbezi juu na Wazo Manispaa ya Kinondoni.
Amesema ujenzi wa barabara hii utakaogharimu fedha za kitanzania shilingi milioni 900 hadi kukamilika kwake, utawasaidia wananchi kuondokana na adha walizokuwa wakizipata hasa ile ya kushindwa kupita na maji kugeuza kuwa njia yake ya kupita.
"Wananchi! tumesikia kilio chenu..... Serikali imekwisha tenga fedha za ujenzi wa barabara hii, tunataka tukiwekeza fedha zetu kwenye barabara zidumu "Amesisitiza Makonda.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo wa barabara kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Mratibu wa TARURA Mkoa huo Eng. George Tarimo amesema barabara ya kinzudi itajengwa kwa muda wa miezi tisa na kazi zitakazofanyika kwenye barabara hiyo ni pamoja na ujenzi wa tuta la barabara, njia za watembea kwa miguu mifereji ya kutolea maji, na kuondoa tabaka la juu lisilofaa.
Kadhalika Eng Tarimo ameainisha changamoto zilizopo katika barabara hiyo kuelekea ujenzi wake kuwa ni wananchi wengi kujenga eneo la barabara, kuingia kwa miundombinu ya umeme, Simu na mabomba ya maji, kunakokwamisha baadhi ya hatua za ujenzi kuendelea.
Awali akiwasalimu wananchi wa Kata ya Mbezi juu, Mkuu huyo wa Mkoa alianisha dhamira na malengo yake mengine ya ujio wake mahali hapo kuwa ni kuhusiana na mradi wa maji unaotoka Ruvu chini, mpango wa kujenga reli ya treni ya kisasa kuanzia wazo kwenda Mwenge, upungufu wa watendaji zahanati ya salasala na kusikiliza kero za wananchi.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano Na habari.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.