Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata zote za Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kuimarisha usafi kwenye Kata zao ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Rai hiyo imetolewa leo tarehe 17 Januari, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Saad Mtambule katika kikao cha Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wote Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kuimarisha masuala ya usafi dhidi ya magonjwa ya mlipuko.
"Leo nimekutana na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata kwa lengo la kujadili namna gani tunaweza kuimarisha usafi kwenye maeneo yetu pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu", amesema Mhe. Mtambule.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.