Wataalamu wa timu za utekelezaji wa mradi wa kuboresha elimu ya awali na msingi "BOOST" kutoka mikoa minne ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na Pwani wamepewa mafunzo ya uelewa wa afua nane muhimu za utekelezaji wa mradi katika mafunzo elekezi yanayoendelea katika Chuo cha Ualimu Morogoro na kuhudhuriwa na wajumbe wa Halmashauri zote za Mikoa husika.
Mafunzo kazi hayo kwa timu za utekelezaji wa mradi wa BOOST yameandaliwa na OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Afua muhimu zilizoanishwa ni pamoja na :-
Aidha, msisitizo umetolewa ili kuhakikisha mahitaji ya msingi ya utekelezaji wa afua yanakamilishwa ili kukidhi vigezo vya kupata msaada wa kifedha kutoka Benki ya Dunia zitakazowezesha kupunguza na kuondoa changamoto mbalimbali za kielimu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini:
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.