Wizara ya Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kutatua changamoto ya mgogoro wa Ardhi uliodumu kwa kipindi cha miaka saba katika eneo la Nyakasangwe Kata ya Wazo kwa kuunda timu itakayofanya tathimini kwa awamu ya mwisho.
Akizungumza na Wananchi wa eneo hilo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wilium Lukuvi amesema kuwa mgogoro huo unaohusisha eneo lenye takribani ekari 2878, umegawanyika katika makundi mawili ambayo ni upande wa wenyemashamba pamoja na wenye makazi wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 3300.
“Nimepokea taarifa ya watalamu wangu lakini bado kunamapangufu kiasi, hivyo nimekuja na timu nyingine kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi Dodoma ambao watafanya kazi kwakushirikiana na Manispaa ya Kinondoni watafika huku muwape ushirikiano, kama mtu ulinunua eneo kwa mtu basi uwe na nyaraka zako” amesema Mhe. Lukuvi
Ameongeza kuwa timu hiyo itaanza kufanya utambuzi kutokana na ripoti ya timu ya awali iliyoundwa na kwamba iwapo itabaini kunauvamizi ulifanyika kwa wanchi hao, serikali haitawavunjia nyumba badala yake watapaswa kulipia gharama ya eneo hilo sambamba na mwenyemashamaba halali na nyumba halali .
Awali akimkaribisha Mhe. Waziri Lukuvi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo alisema kuwa kwasasa Manispaa ya Kinondoni imefanikiwa kupima viwanja takriban 9000, hali iliyopelekea kupunguza migogoro hiyo kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Chongolo amesema Wananchi ambao tayari wameshapimiwa viwanja vyao wanapaswa kuchukua hati zao sambamba na wale ambao maeneo yao hajapimwa kuchukua hatua ili kuepukana na usumbufu wowote unaoweza kujitokeza.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.