Timu ya wataalamu kutoka Benki ya dunia leo wamefanya ziara kutembelea miradi inayogharamiwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu, na mkopo kutoka Benki ya Dunia chini ya mradi wa uboreshaji Jiji la Dar Es Salaam (DMDP) inayotekekezwa katika Manispaa ya Kinondoni.
Timu hiyo chini ya uongozi wake Mr Eric imetembelea miradi inayotekelezwa kwa awamu tatu tofauti kwa lengo la kuangalia hatua za utekelezaji, maswala ya Mazingira ,maswala ya fidia, pamoja na athari wazipatazo wananchi katika kutekeleza miradi hiyo.
Katika awamu ya kwanza miradi iliyokaguliwa ni ile miradi inayiendelea na ujenzi ambazo ni barabara ya Makumbusho yenye urefu wa Km 1.45, MMK km 0.69, Nzasa ni km 1.25, Viwandani ni km 2.1,Tanesco soko la Samaki ni km 1.67,pamoja na ujenzi wa ofisi iliyoko eneo la bustani ya Magomeni.
Miradi itakayotekelezwa kwa awamu ya pili ambayo yenyewe bado haijaanza ni ujenzi wa barabara ya Makanya km 5.1, Ujenzi wa barabara ya Sim 2000 yenye urefu wa km 1.3, ujenzi wa barabara ya Kilimani urefu wa km 1.3, barabara ya Tandele kisiwani urefu km 0.4, na barabara ya kilongawima yenye urefu wa km 2.1.
Awamu ya tatu nayo itahusisha barabara ya External yenye urefu wa km 2.65, barabara ya Kisukulu yenye urefu wa km 1.9 na barabara ya korogwe kilungule yenye urefu wa km 2.88
Akizungumnzia changamoto za utekelezaji wa miradi hiyo Mratibu wa Mradi kutoka Manispaa ambaye pia ni mhandisi wa barabara Ndugu Mkelewe Tungaraza amesema ucheleweshwaji wa kuondolewa kwa mabomba ya maji safi na maji taka sehemu zinazojengwa barabara, wanachi waliojenga kwenye hifadhi ya barabara kushindwa kuondoa Mali zao, pamoja na kutiririshwa kwa maji kutoka viwandani kinyume cha utaratibu.
Timu hiyo pia iliambatana na wataalam kutoka Manispaa,ikihusisha wahandisi washauri wa miradi kutoka kampuni ya GAUFF, Kampuni shauri inayojengea wataalam wa Manispaa uwezo iitwayo LATTANZIO, pamoja na mkandarasi kutoka kampuni ya Esteem.
Imetolewa na
Kitengo cha Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.