Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshiwa Godwin Gondwe alipozuru eneo la mafuriko Kunduchi na kujiridhisha na hali ya uharibifu iliyosababishwa na mvua zilizonyesha.
Amesema kufika kwake eneo hilo la mafuriko Kunduchi ni kutokana na malalamiko mengi aliyoyapata kwa wananchi wake kufuatia adha ya mafuriko wanayoipata kipindi cha mvua.
Ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni Serikali sikivu inayolenga kutatua kero za wananchi zinazowakabili kwa wakati na ufanisi hali itakayoleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
"Kwanza wazo la kutengeneza mfereji huu Serikali imeshalichukua tayari na kwamba Mfuko wa Barabara "Road fund", unalifahamu tayari na kwamba kuna fedha wanatakiwa kuzitoa kwa ajili ya kutengeneza huu mfereji mkubwa ambao ndio mahangaiko makubwa kwa wananchi kutoka kule Pwani mpaka Basihaya ili watu wasisumbuke na mafuriko" Amefafanua, Godwin Gondwe.
Amewataka wananchi wa Kunduchi kusimamia kwa umakini eneo la barabara lisivamiwe mara baada ya kutengenezwa mifereji itakayosaidia kuzuia uharibifu wa mafuriko kutoka Pwani mpaka Basihaya.
Katika hatua nyingine amewataka Wakala wa Barabara Tanzania "TANROADS" kuhakikisha wanakamilisha mchoro na utafiti utakaolekeza njia nzuri ya maji kwenda baharini.
Katika ziara yake hiyo Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alitembelea miradi ya shule, zahanati na barabara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake katika kutembelea miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano.
Manispaa ya Kinondoni.
2 Barabara ya Morogoro, 14883 Dar es Salaam
Anuani ya Posta: S.L.P 31902
Simu ya mezani: +255222170173
Simu ya mkononi: +255733241052
Barua pepe: md@kinondonimc.go.tz
Hatimiliki © 2017 Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Haki Zote Zimehifadhiwa.